2 Samuel 5:11-16

11 aBasi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, maseremala na waashi, nao wakajenga jumba la kifalme kwa ajili ya Daudi. 12 bNaye Daudi akafahamu kuwa Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na ameinua ufalme wake kwa ajili ya Israeli, watu wake.

13 cBaada ya Daudi kuondoka Hebroni, akajitwalia masuria zaidi na wake huko Yerusalemu, nao wana na binti wengi walizaliwa kwake. 14 dHaya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Sulemani, 15Ibihari, Elishua, Nefegi, Yafia, 16Elishama, Eliada na Elifeleti.

Daudi Awashinda Wafilisti

(1 Nyakati 14:8-17)

Copyright information for SwhKC